Takukuru Songwe Yaokoa Nyumba ya Mama Mjane

Taasisi ya Kuzuia na Kudhibiti Rushwa mkoani Songwe, (Takukuru) imefanikiwa kumrejesha Mama mjane hati yake ya nyumba iliowekwa rehani kwa deni la mumewe.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Songwe, Kamanda wa Takukuru mkoani humo, Damas Suta alisema kwamba Septemba 02, 2020, mjane aitwae Agnes Mwakatole alifika ofisi za Takukuru na kudai kuwa Jeradi Kombe alimkopesha marehemu mumewe Adam Mwakatole kiasi cha Sh milioni 15.

Aliendelea kufafanua kuwa baada ya mumewe kufariki Jerard Kombe alibadili deni hilo na kulipandisha hadi milioni 40 kiasi ambacho alitaka alipwe au achukua nyumba yao iliyokuwa imewekwa rehani kama dhamana na mumewe.


Kamanda Suta alisema baada ya kujiridhisha kuwa mkopo huo ulikuwa umekiuka sheria za nchi, ofisi ya Takukuru ilimtaka Mama huyo kumlipa Jerard Kombe kiasi cha milioni 15 ambayo ndio mkopo halali aliokuwa anadai marehemu mumewe.

Pia walimtaka Jerard Kombe kupokea kiasi hicho na kumrejeshea mama huyo hati yake na makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya Kamanda Suta.

NA MWANDISHI WETUToa comment