Tamasha La Waimba Injili Kuombea Uchaguzi Mkuu Laahirishwa

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akitangaza kuahirisha tamasha hilo.

Tamasha la waimba injili lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion na kwa ajili ya kuuombea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu limeahirishwa mpaka hapo litakapotajwa tena.

Wanahabari kazini kwenye mkutano huo.

Tamasha hilo lilitakiwa kufanyika septemba 6 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwa leo Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama amesema tamasha hilo limeahirishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Msama baada ya kuahirisha tamasha hilo.

 

Akitaja baadhi ya sababu hizo Msama alisema ni kuambiwa wakitakia kufanya tamasha hilo limalizike saa kumi na mbili jioni muda ambao tamasha lingekuwa limeanza kunoga.

Sababu hiyo na nyinginezo ndizo zilizosababisha kuahirishwa kiwa tamasha hilo.

Rose Muhando ambaye alitakiwa kuwaongoza waimba injili wenzake.

Awali Msama alimtambulisha gwiji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando na kusema ndiye ambaye angewaongoza waimbaji wenzake.

HABARI/PICHA: WAANDISHI WETU  Toa comment