TAMNOA Washiriki Warsha Kujadili Mbinu Za Kudhibiti Utapeli Kwa Simu

Katika warsha hiyo iliyoandaliwa na GSMA, kupitia mtandao au webinar, wawakilishi kutoka makampuni ya simu waliweza kuchangia mada mbalimbali. Kutoka Tigo alikuwepo Nkata Kagoma, wengi walikubaliana kwamba utapeli ni tatizo kubwa Barani Afrika, na wateja wanahitaji kupata elimu kuhusu tahadhari mbalimbali wanazoweza kutumia kuzuia utapeli kwa njia za simu za mkononi, pia wengi walikubaliana kuwa teknolojia ya dijitali inaweza ikasaidia kutatua matatizo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika jamii ikiwa itapewa msukumo wa aina yake.

 Toa comment