Tanasha: mahari Yangu Inakuja Soon

STAA wa muziki kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna Oketch, amefunguka kuwa, hivi karibuni anaweza kutolewa mahari na kuwa mke wa mtu.

 

Tanasha amewaacha watu midomo wazi baada ya kumjibu hivyo shabiki ambaye alizungumzia ishu ya yeye (Tanasha) kutokutolewa mahari na aliyekuwa mchumba’ke, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Tanasha aliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa; “Wazee wangu kutoka homebay watakuwa wananihitaji zaidi…’’

 

Baada ya kuandika ujumbe huo, shabiki anayejiita Frorence Akoth alijibu; “Tanasha hebu acha hivyo vitu, mimi pia natoka homebay, wewe ulituangusha hata mahari haikuletwa…”

 

Kwa upande wake Tanasha alirejea na kumjibu shabiki huyo kuwa, mahari inakuja nyumbani soon. “Usijali bwana coming soon,’’ alijibu Tanasha. Baada ya kujibu hivyo, wapo walimpongeza kwa hatua hiyo kubwa ambayo inakwenda kutimia hivi karibuni.

 

“Piga kelele kwa biharusi wake wewee,’’ aliandika shabiki mmoja kwenye ukurasa wa Tanasha. Mbali na kuwa mzazi mwenza wa Diamond au Mondi, Tanasha amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na jamaa kutokea nchini Kenya anayejulikana kwa jina la Jamal, ambaye inasemekana ni meneja wake.

 

Tanasha ni mrembo ambaye amezaa na Mondi ambapo wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Naseeb Juniour.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DARToa comment