TANZIA: Aliyekuwa Mwandishi na Mtangazaji wa ITV Agnes Almasy, anatarajiwa kuagwa kesho na kupelekwa Tanga kwa mazishi

4 0

Akizungumza kwa niaba ya Familia, Shangazi wa marehemu Rose Almasy, amesema kuwa marehemu Agnes ataagwa kesho katika kanisa la Anglican Buguruni na baadaye wataanza safari ya kuelekea Tanga.

“Maandizi yanaendelea baina yetu familia pamoja na kampuni aliyokuwa akifanyia kazi, tutampumzisha mpendwa wetu Tanga”, Shangazi yake Agnes.

Marehemu Agnes ameacha mume na mtoto mmoja wa kike.

Agnes alihitimu Stashada katika Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam, ambapo baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Lovely Proffesional University kilichopo nchini India na kupata Shahada ya Uandishi wa Habari na Umma mwaka 2017.

Agnes aliajiriwa rasmi katika kituo cha utangazaji cha ITV Machi 19, 2018 kama Mwandishi wa Habari.

Mungu ailaze roho ya marehemu Agnes Almasy mahali pema. Amina

Chanzo Eatv.tv.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *