Tanzia: Dr Shika Afariki Dunia

Dr Louis Shika maarufu kama Mzee wa 900 Itapendeza amefariki dunia, akiwa nyumbani kwa kaka yake wakati wa uangalizi baada ya matibabu katika Hospital ya Nyanguge iliyopo Wilayani Magu nje kidogo ya Jiji la Mwanza.

Awali Dr Shika Aalikuwa amelazwa Hospitali hapo kwa muda mrefu akipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya figo.

Global Publishers tumezungumza na daktari kutoka Hospitalini hapo ambaye allikuwa akimtibu na kuthibitisha kuwa Dr Shika amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

“Alikuwa akitibiwa hapa kwa mrefu lakini baadaye alipata nafuu tukamrusuhu akawa nyumbani kwa kaka yake kwa ajili ya uangalizi, lakini hali yake ilibadilika ghafla jana asubuhi, nilifika mapema kwa ajili ya kumhudumia lakini haikuchukua muda akawa amefariki majira ya saa 5 asubuhi.” – amesema Daktari.

Taarifa zaidi tutakuletea hapa, ila taarifa zaidi zinasema kuwa msiba upo kwa kakabyake hapo hapo Nyanguge na mazishi yake yanatarajiwa kutfanyika kesho.

Taarifa zaidi tutaendelea kukujuza.

 Toa comment