TANZIA: Mfahamu Mwanasiasa mkongwe na mwanzilishi wa chama cha CUF aliyepoteza maisha

5 0

Mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki alikokuwa amelazwa kwa wiki 2 akipatiwa matibabu baada ya kusumbuliwa na maradhi katika mfumo wa upumuaji.


James Mapalala alizaliwa mnamo, Februari 1 mwaka 1936. Mtoto wake, Bernard James amesema Baba yake amefariki dunia alfajiri ya leo na msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Kinondoni

Alianza harakati za siasa mnamo mwaka 1968 wakati huo.

MWANASIASA mkongwe nchini Tanzania na mwanzilishi wa Chama cha Wananchi, Mzee James Mapalala amefariki dunia jana Jumatano Oktoba 23, 2019, saa 4:30 asubuhi katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa taarifa ya mtoto wake Bernard James amethibitisha kutokea kwa kifo cha mzee huyo na kueleza kilichokuwa kinamsumbua kwa alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Kairuki tangu wiki mbili zilizopita kwa kuwa alikuwa  akisumbuliwa na maradhi ya kupumua.

 

“Alikuwa hospitali tangu wiki mbili zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupumua. Familia imekusanyika nyumbani Kinondoni kupanga ratiba ya mazishi,”.

Mapalala aliyezaliwa Februari Mosi, 1936 ameacha mke na watoto kadhaa. Alikuwa miongoni mwa wanasiasa wa kwanza waliojitosa kudai mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini Tanzania.

Kufuatia madai hayo, Mapalala alifungwa miaka miwili mkoani Lindi kuanzia mwaka 1986 hadi 1989 na baada ya kutoka aliwekwa kizuizini kwa kipindi cha mwaka mmoja katika kisiwa cha Mafia baada ya kuanzishwa chama cha siasa wakati sheria ilikuwa hairuhusu.

Alianzisha Chama cha Wananchi (CCW) mwaka 1991 na baadaye kiliungana na chama cha Zanzibar – Kamahuru na mwaka 1993 kuzaliwa Chama cha Wananchi (CUF).

By Ally Juma.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *