Tanzia: Mtangazaji wa ITV Agnes Almas Afariki Dunia

MWANDISHI wa habari na mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV, Agnes Almas,  amefariki dunia ghafla mchana wa leo Alhamisi, Septemba 3, 2020, akiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam baada ya kujisikia vibaya alipokuwa nyumbani kwake akijiaandaa kwenda kazini.

 

Radio One na ITV Tanzania wamethibitisha kutokea kwa msiba huo kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii.

#TANZIA: Tunasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu Agnes Almas @ITVTANZANIA. R.I.P AGNES ALMASY.” wameandika ITV kupitia akaunti yao ya Twitter.Toa comment