Tanzia: Mwanasiasa Mkongwe, Balozi Lusinde Afariki Dunia

Mwanasiasa mkongwe, Balozi Job Lusinde (90) ambaye aliunda baraza la kwanza la Mwalimu Julius Nyerere baada ya uhuru amefariki dunia alfajiri ya leo Jumanne, Julai 7, 2020, katika Hospitali ya Mloganzila jijiniu Dar es Salaam.

 

Familia ya Lusinde na Malecela imesema taratibu za mazishi zinaendelea katika makazi yake, Kilimani, jijini Dodoma. Lusinde ni kaka wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, John Malecela.

 

Lusinde aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano mwaka 1965 na ni miongoni mwa watu walio fanya kazi kwa ukaribu na Mwalimu Julius Nyerere kama Waziri wa Serikali za Mitaa mwaka 1961. Pia, aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini China kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1984.

 Toa comment