Tanzia: Rais Pascal Lissouba Afariki Dunia

Rais wa zamani wa Congo/Brazaville Pascal Lissouba, amefariki dunia nchini Ufaransa akiwa na umri wa miaka 88, chama chake kimeliambia shirika la habari la AFP.

 

“Rais Lissouba amekufa baada ya kuugua,” Mbunge na msemaji wa chama cha Pan-African Union for Social Democracy (UPADS) Honore Sayi amesema.

 

Kifo chake pia kimethibitishwa kwenye ukurasa wa Facebook na mwanae wa kiume Jeremie Lissouba, ambaye pia ni mbunge.

 

Bwana Lissouba mbaye alishinda katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingimwaka 1992, alitoroka nchi yake na kwenda Ufaransa baada ya kupinduliwa na rais wa sasa Denis Sassou Nguesso, ambaye alishindwa katika uchaguzi huo.Toa comment