Tanzia: Rais wa Ngumi za Kulipwa Tanzania Afariki

RAIS wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa nchini Tanzania (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustadhi’, amefariki dunia asubuhi ya leo, Septemba 7, 2020 nyumbani kwake Buza Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda.

Yassin atakumbukwa kwa msimamo wake wa kuwatetea mabondia wa ngumi za kulipwa nchini na kuutangaza mchezo huo.
Inna Lillah Wayna Illaih Rajiun.Toa comment