TCAA Yazuia Mashirika 3 ya Ndege Kenya Kufanya Safari TZ

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezizuia kampuni tatu za ndege kutoka Kenya, ambazo ni Air Kenya Express, Fly 540 na Safarilink Aviation kufanya safari zake nchini kutokana na mvutano unaoendelea baina ya nchi hizo hasa sakata la Covid-19.

 

Hii imekuja ikiwa ni wiki chache baada ya Kenya kutangaza nchi 130 ambazo wananchi wake wanaruhusiwa kuingia nchini humo bila masharti ya kuwekwa karantini ya siku 14 wakati Watanzania wanaoingia Kenya wakitakiwa kuwekwa karantini.

Juzi Jumanne, TCAA ilifuta vibali vya Fly 540, Air Kenya Express na Safarilink Aviation, kufanya safari zake nchini. Ndege hizo hufanya safari zake kila siku kati ya Kilimanjaro na Zanzibar.

 

Agosti 1, 2020, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imefuta kibali kilichokuwa kikiruhusu ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kutua Tanzania, uamuzi huo umekuja baada ya Kenya kutoijumuisha Tanzania katika orodha ya Nchi ambazo Raia wake wataruhusiwa kuingia Kenya kuanzia Agosti 01. Ndege za Kenya zilisitishwa kutua katika uwanja wa ndege wa JNIA – Dar es Salaam, KIA – Kilimanjaro, wala AAKIA – Zanzibar.

“Reference is made to the approval for your summer schedule application extended to Air Kenya Express. The approval was granted to Air Kenya for schedule flight operations between Nairobi and Kilimanjaro with effect from March 27 to October 25. However, we regret to inform you that this approval is hereby nullified,” TCAA director-general Hamza Johari said in the letter to Air Kenya’s operations manager.

TCAA did not give any reasons as to why it was nullifying the approvals, only informing the privately-owned Kenyan airlines that this notice now rescinds any previous approval allowing it to fly to Tanzania.

 

“You will therefore be allowed to apply afresh for any operations into Tanzania before consideration can be made. It was surprising that Tanzania, whose President John Magufuli declared it Covid-19 free, is exempted from the list. What message are they sending to the world about Tanzania?” Mr Johari added.Toa comment