Terry: Chelsea msimwache Sancho – Gazeti la Dimba

11 0


LONDON, England

KWA ushauri wa beki mkongwe, John Terry, timu yake ya zamani, Chelsea, inatakiwa kufanya kila linalowezekana kuipata saini ya kinda wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho.

Alichokisema Terry, ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa Aston Villa, kuongezeka kwa Sancho kutakiimarisha kikosi cha Chelsea.

Sancho mwenye umri wa miaka 19, amekuwa akihusishwa na klabu za Ligi Kuu ya England (EPL) kutokana na kiwango kizuri alichonacho kule Bundesliga.

Licha ya kuwasifia makinda waliopo Stamford Bridge, akiwataja Tammy Abraham na Mason Mount, Terry alisema: 

“Nafikiri Sancho ni mmoja kati ya makinda bora duniani kwa sasa na ataongeza kitu kwenye kikosi cha Chelsea na kutufanya bora zaidi.”Source link

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *