Tetesi za usajili barani Ulaya, ruksa Messi kuondoka Barcelona msimu ujao bila malipo, Madrid yahamia kwa Mbappe

23 0

Lionel Messi ataruhusiwa kuondoka Barcelona bila malipo yoyote msimu ujao , iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atapendelea kufanya hivyo kutokana na kifungu cha sheria katika kandarasi yake.

(El Pais, via L’Equipe). Messi ataruhusiwa kuzungumzia hatma yake na klabu yoyote kutoka Januari mosi. (Marca – in Spanish).

Kylian Mbappe

Real Madrid itamwania mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe msimu ujao .

Mabingwa hao wa Ufaransa waliwaonya Barcelona kuhusu lengo hilo la Real Madrid wakati wa mazungumzo ya vilabu hivyo viwili kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu huu.. (Sport – in Spanish)

Neymar JnrHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Brazil Neymar atalazimika kusalia PSG hadi pale atakapokubali kupunguza marupurupu yake kulingana na rais wa La Liga Javier Tebas. (Mail)

Chris Smalling yuko tayari kuondoka Man United baada ya beki huyo mwenye umri wa miaka 28 kujiunga na klabu ya Roma kwa mkopo. (Mirror)

Marcus Rojo

Na Beki wa United raia wa Argentina Marcos Rojo, 29, yuko tayari kupigania uhamisho wa mwezi Januari mbali na klabu hiyo iwapo atahitajika kufanya hivyo baada ya uhamisho wake wa kuelekea Everton kugonga mwamba. (Ole – in Spanish)

Mabingwa wa Itali Juventus wanafikiria kumnunua beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30, na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27.

Tobby Alderwield

Inter Milan pia wana hamu ya kumsajili Alderweireld. (Mail)

Mabingwa wa Uhispania Barcelona walitaka kumsaini winga wa Itali mwenye umri wa miaka 25 Federico Bernardeschi kutoka Juventus katika dirisha la uhamisho la msimu huu (Mundo Deportivo – in Spanish)

By Ally Juma.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *