TGNP Yatoa Semina ya Kujadili Bajeti ya Mlengo wa Kijinsia

Wadau wakiwa makini kwenye semina hiyo.

Taasisi ya Mtandao wa Jinsia (TGNP) yafanya semina kujadili ufahamu wa wadau kuhusu bajeti inayotengwa  kwa ajili ya watu kwenye mlengo maalum. Wadau walihudhuria semina hiyo wameelezea namna wanavyofahamu kuhusu bajeti hiyo na inazungumzaje kuhusu kunufaika kwa watu wenye mlengo wa kijinsia.

Akizungumza mapema leo kwenye semina ya maendeleo ya jamii (GDSS) mwezeshaji wa uwekezaji na jinsia, Thabitha Elias amesema kuwa malengo mbalimbali za kijinsia, uchambuzi wa kijinsia ni mchakato ambao unaweka bayana mpango wa kijinsia.

“Mnyambuliko wa kijinsia ambao hukusanya data ili kuweza kujua ni namna gani jamii itawezeshwa katika mambo mbalimbali ikiwemo maji, elimu na mambo mengi yanayohusisha wakina mama.

Mwezeshaji wa uwekezaji na jinsia, Thabitha Elias akitoa somo.

Nae Afisa Program, Idara ya Habari na Mawasiliano (TGNP), Jackson Elias amesema kuwa jamii inatakaiwa iwe inafika katika ofisi yao ili kujua na kuchangia bajeti iliyotengwa ili inapopelekwa kujadiliwa iweze kukidhi mahitaji ya walengwa.

“Bajeti ambayo inatengwa kwa ajili ya watu wenye mlengo wa kijinsia itasaidia kujua changamoto zao ambapo bila kufanya hivyo ikishafika kipindi cha bajeti ya serikali wanaweza kukuta bajeti kwa upande wao haiwatoshelezi lakini wakifika na kutoa maoni yao hiyo itasaidia kuwafikiria mapema”. Alimaliza kusema Jackson.Toa comment