Tid: Corona Isiwe Kiki!

BAADA ya dunia na nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania kukumbwa na janga zito la virusi vya Corona na baadhi ya mastaa kujitangaza kuwa na virusi hivyo, msanii wa muziki wa Bongo Fleva; Khaled Mohamed ‘Tid’, amefunguka kuwa watu wasitumie janga hilo kama njia ya kufanya kiki.

 

Tid amesema kuwa watu wamekuwa wakitumia janga hilo ambalo linaendelea kuathiri watu wengi kama njia ya kujionesha wao wenyewe na mambo yao binafsi.

 

“Nina miaka ishirini katika tasnia hii ya muziki, nafanya muziki na kuelimisha jamii. Suala la Corona kuna watu wengine wanataka kutumia kama advantage wao kuonekana kama mfano, inapaswa tujue ni janga kubwa ulimwenguni kote na hata wasanii linatuathiri vibaya, watu wajue hili ni tatizo serious si la mtu kujiongelea, mbona mimi najua watu wengi wako karantini lakini sijatangaza, cha msingi ni kuzingatia maelekezo tu na si vinginevyo,” alisema Tid bila kuwataja majina wahusika.

STORI: KHADIJA BAKARI
Toa comment