TMA Yatabiri Upungufu wa Mvua

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, Novemba na Desemba unaonyesha kwamba maeneo mengi ya nchi yatapata mvua chache na hivyo kusababisha athari ikiwemo upungufu wa chakula.

Β 

Mkurugenzi mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema hayo leo jijini Dar es salaam na kuwashauri wakulima kupanda mbegu za mazao ambazo zinakua hazihitaji maji mengi.

Β 

Dkt. Kijazi pia ameeleza kuwa athari hizo zitajitokeza si kwa Tanzania pekee bali pia ni kwa nchi zote za Afrika Mashariki huku akieleza athari hizo kwa sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo wafugaji na wakulima.Toa comment