Tokomeza Corona ya Championi, Spoti Xtra Yatinga Karume, Buguruni

GLOBAL Publishers kupitia magazeti yake bora ya michezo Tanzania ya Championi na Spoti Xtra, imeendelea na kampeni ya kuzuia kusambaa kwa Virusi vya Corona na kuvitokomeza kabisa.

 

Katika kampeni hiyo, leo Ijumaa, timu ya Global Publishers ilitembelea mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuweka ndoo maalum za maji ambapo watu watakuwa wakinawa katika kujikinga na Corona.

Baadhi ya mitaa ambayo timu ya Global Publishers ilitembelea ni Kituo cha Daladala cha Manzese na soko la Karume Ilala na Soko la Buguruni.

Baada ya kuwekwa kwa ndoo hizo za maji, watu mbalimbali wakawa mstari wa mbele katika kunawa ili kuungana na Global Publishers kutokomeza Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

 

 

 

 
Toa comment