Trump Ashtukia Kuibiwa Kura, Akionya Chama Chake!

2 0Trump Ashtukia Kuibiwa Kura, Akionya Chama Chake!

Rais wa Marekani Donald Trump amewaonya Warepublican wenzake kwamba wapinzani wao huenda “wakaiba” uchaguzi wa Novemba, wakati chama chake kilipomuidhinisha kuwa mgombea wao.

 

“Wanatumia Covid 19 kuwalaghai Wamarekani,”Bw. Trump aliwaambia wajumbe katika siku ya kwanza ya kongamano la chama chake huko North Carolina.

 

Bwana Trump alirudia kauli hiyo tata akidai kuwa upigaji kura kupitia sanduku la posta utachangia udanganyifu. Kura za maoni zinaonesha kuwa mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden anaongoza.

 

Akiwahutubia wajumbe moja kwa moja katika mkutano mkuu wa chama ambao umepunguza idadi ya watu waliohudhuria kutokana na Covid-19, Bwana Trump aliwalaumu wafuasi wa chama cha Democrats kwa “kutumia Covid kufanya udanganyifu katika uchaguzi”.Trump aliteua- jamaa zake kwa wingi katika kuratiba ya mkutano huo.

 

“Njia pekee wanaweza kutushinda katika uchaguzi huu ni kufanya udanganyifu,” alisema. “Tutashinda.”

Bw. Trumpa pia alionya ”udanganyifu” katika uchaguzi wa 2016, alipokuwa nyuma ya Hillary Clinton katika kura ya maoni.

 

Kama ada, Bwana Trump aliteuliwa rasmi kuwa mgombea wa Republican siku ya Jumatatu katika mkutano mkuu wa chama chake mjini Charlotte. Rais huyo anatarajiwa kuhutubia mkutano wa kongamano la chama chake siku ya Alhamisi. Sio kawaida kwa mgombea kuhutumia wajumbe kabla ya kutoa hotuba rasmi ya kukubali uteuzi.

 

Wafuasi katika mkutano huo walishangilia kauli ya Bwana Trump, na kuanza kuimba kwa pamoja “miaka minne zaidi” Bwana Trump aliwakatiza kwa kusema.

 

“Sasa mkitaka kuwatia wazimu, semeni miaka 12 zaidi,” alisema. Marekebisho ya 22 ya Katiba ya Marekani, iliyoidhinishwa 1951, inasema marais wa Marekani wanaruhusiwa kuhudumu kwa mihula miwili ya miaka ya miaka minne kwa jumla.

 

Je upigaji kura kupitia posta ni salama?
Bwana Trump amerudia mara kadhaa kwamba upanuzi wa zoezi la kupiga kura kupitia njia ya posta – hali ambayo itashuhudiwa zaidi mwaka huu kutokana na janga linaloendelea la corona – litachangia “ufisadi mkubwa” katika historia ya Marekani.

 

Lakini hakuna ushahidi wa udanganyifu ulioshuhudiwa, na ukweli ni kwamba ni Wamarekani wachache kwa mfano wameshitakiwa kutokana na uhalifu huo. Ellen Weintraub, Kamishna wa Tume ya Kitaifa ya Uchuguzi, amesema: “Hakuna msingi wowote wa njama kwamba upigaji kura kupitia sanduku la posta unaweza kusababisha ulaghai. Hakuna.”

 

Upigaji kura kupitia sanduku la posta umekuepo tangu zama za vita nichini Marekani, na ulitumiwa na wanajeshi nchini humo, Bwana Trump mwenyewe na familia yake. Lakini kupunguzwa kwa mpango wa kuwapelekea watu barua nyumbani kama hatua ya kubana matumizi katika idara ya posta Marekani.

 

Kumekuwa na hofu huenda kura zitakazopigwa kupitia mfumo huo zisirudishwe kwa maafisa wa kitaifa siku ya uchaguzi.

 

Majimbo kadhaa yanataka kubadilisha sheria za uchaguzi ili kuruhusu kura kuhesabiwa siku kadhaaa baada ya uchaguzi wa urais, pendekezo ambalo wachambuzi wanahofia litachelewesha kuamua mshindi wa urais.

 

Uchaguzi wa wagombea mjini New York mwezi Juni ulichukuwa wiki kadhaa kuamua mshindi baada ya maafisa wa uchaguzi kuchanganya mara 10 nambari za kura zilizopigwa kupitia sanduku la posta.

 

Hakukutokea madai ya ulaghai, lakini mchanganyiko huo umeibua hofu kwamba shughuli za kuhesabu kura itachukua muda mrefu zaidi Katika uchaguzi wa Novemba.

 

Mapema mwezi huu, maafisa New Jersey waliamuru uchaguzi ufanyike upya baada ya kupata ushahidi kwamba kulikuwa na udanganyifu wa kura katika kura zote zilizopigwa kupitia mfumo wa posta katika sakata iliyosababisha watu wanne kukamatwa. Kesi hiyo imekuwa ikiangaziwa na kampeini ya Trump.Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *