Tshishimbi Aikubali Simba

NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi raia wa DR Congo, amebainisha kuwa kwa mechi zilizobaki na pointi ambazo wamezidiwa na wapinzani wao Simba, hakuna nafasi ya wao kuwafi kia.

 

Tshishimbi amesema kwa hali halisi ilivyo kwa sasa katika Ligi Kuu Bara, ni ngumu kwao kutwaa ubingwa huo ambao wameukosa kwa misimu miwili mfululizo.

 

Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 51, wamepitwa pointi 20 na Simba wanaongoza ligi hiyo wenye pointi 71. Yanga imebakiwa na mechi 11, Simba mechi kumi.

 

“Sidhani na wala siyo rahisi kutwaa ubingwa kwa msimu huu. Mechi zimebaki chache na pointi walizotuzidi Simba ni nyingi. Ni ngumu sana kuwapata,” alisema Tshishimbi.
Toa comment