tujiandae kwa Oktoba 28 – Dar24

3 0

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amewaomba wananchi wa mkoa wa Pwani kuhakikisha wanachagua Rais, wabunge na madiwani wanaotoka katika chama hicho watakaosimamia haki na uhuru.

Ametoa ombi hilo wakati akizindua kampeni za chama hicho mkoa wa Pwani, ambapo amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza nchi ataunda serikali ya uhuru na maendeleo.

“Nawaombeni wote tujiandae kwa Oktoba 28, tuhakikishe tunachagua madiwani watakaosimamia haki badala ya kunyamaza, chagueni Mbunge wa CHADEMA atakayepiga kelele Bungeni,” amesema Tundu Lissu.

Baadaye leo Septemba 11,2020, Lissu ataendelea na kampeni zake katika mkoa wa Morogoro.

“Jukumu la ulinzi na usalama wa nchi yetu ni letu sote”
EU kugongelea msumari vikwazo dhidi ya Uturuki

Comments

comments

Posted from

Related Post

Sevilla wamzuia Messi mabao 700

Posted by - June 21, 2020 0
CATALUNYA, Hispania SULUHU ya juzi dhidi ya Sevilla yalimzuia Lionel Messi kufikisha mabao 700 tangu aanze kucheza soka la kulipwa.…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *