Tuyisenge Aaga Rasmi Luanda, Yanga Washindwe Wao Tu

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Petro de Luanda anayetajwa kuwindwa na Yanga, Jacques Tuyisenge kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, ameiaga rasmi familia ya waajiri wake wa zamani baada ya kuvunja mkataba na timu hiyo kwa madai ya kuhitaji changamoto mpya.

Yanga inatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la usajili wa Tuyisenge ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo ilionekana kuwa tatizo kubwa msimu uliopita.

 

Taarifa rasmi aliyoiposti mchezaji huyo kwenye akaunti yake ilikuwa na picha ya kikosi cha Petro de Luanda na kusindikizwa na maneno:“Nashukuru sana kwa kupata fursa ya kuwa sehemu ya familia ya Peter de Luanda, imekuwa uzoefu mzuri nanyi wote, asante kwa kunipa nafasi ya kutimiza uwezo wangu hapa. Nawatakia mafanikio mema katika mwendelezo wa safari inayoendelea.

Joel Thomas,Dar es SalaamToa comment