Uchaguzi Tanzania 2020: Magufuli amwacha mbali Lissu katika matokeo ya awali

25 0

Matokeo ya uchaguzi kwa ngazi ya urais yanaendelea kutangazwa nchini Tanzania huku rais aliye madarakani na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiongoza katika matokeo ya awali.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Magufuli anaongoza kwa asilimia 84.8 katika matokeo ya majimbo 202 yaliyotangazwa matokeo yake na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufikia sasa.

Mgombea wa Chama kikuu cha upinzani Chadema Tundu Lissu ana asilimia 12.5%.

Tanzania ina majimbo 264 ya uchaguzi hivyo bado matokeo ya majimbo 62 tu ili matokeo rasmi yatangazwe.

Hata hivyo, Lissu ametangaza kutoyakubali matokeo ya uchaguzi wa Jumatano akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu pamoja na mawakala wa upizani kuzuiwa kuingia vituoni.

Lakini madai hayo yametupiliwa mbali na NEC.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *