Uingereza: Waziri Mkuu Boris Johnson Apata Corona

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amethibitika kuwa na virusi vya corona, taarifa iliyotolewa na Mamlaka za Uingereza imesema Boris atalazimika kujitenga ili kuepusha kuwaambukiza wengine.

 

Boris kupitia ukurasa wake wa Twitter, amethibitisha kuwa na maambukizi ya virusi vya corona na dalili za  #Covid-19 na kusema yupo karantini na ataendelea kuwa kiongozi wa serikali katika kupambana na janga hilo la Covid-19 Uingereza.

 

“Nilipata dalili za homa nimepimwa nimekutwa na virusi vya corona, kwa sasa nimejitenga ila tupo kwenye Dunia ya teknolojia nitaendelea kuongoza Serikali na kuwajibika kupitia video conference wakati huu ambapo tunapambana na corona,” amesema Boris Johnson.

 

 
Toa comment