Ukaribu wa Harmonize Killy na Cheed waliotoka kwa Alikiba wazidi, huenda wakatambulishwa Konde Gang

5 0

Hali hiyo imekuja baada ya Killy na Cheed kupost matukio ambayo anayafanya Harmonize kwenye kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram, huku watu wakiwatarajia huenda wao ndiyo wakawa wasanii wapya wa lebo ya Konde Gang.

Pia ukifuatilia post yao ya mwisho kabla ya hiyo ya jana, Cheed na Killy wote walishea post ya video mpya ya Harmonize iitwayo Jeshi kwenye kurasa zao za Instagram.

Ukifuatilia tukio la Harmonize kwenye kilele cha siku ya Wananchi Uwanja wa Benjamin William Mkapa, msanii Killy alimpost Harmonize akiwa amevaa mavazi ya kijeshi kisha kuandika “Mmakonde mmoja”.

Baada ya kuandika ujumbe huo Harmonize alikuja kwenye page ya Killy na kucomment my Gee 4 ever na Killy ku comment akiweka emoji ya tembo.

Mbali na hilo Harmonize alitangaza kutambulisha wasanii watatu mwezi wa nane na badala yake alitambulisha mmoja ambaye ni Skales kutoka Nigeria, swali ni je waliobaki wawili ambao hawajatambulishwa bado huenda ikawa ni Cheed na Killy waliotoka Kings music lebel kwa Alikiba?

Unahisi Cheed na Killy wanaweza kutambulishwa Konde Gang na Harmonize ?

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *