Ukoo wa Laizer waendelea kukusanya mamilioni, mwingine huyu alamba milioni 267

2 0

Kampuni ya Michezo na Burudani ya SportPesa Tanzania imemkabidhi mshindi wa Jackpot SportPesa , Lilian Ngitoria Laizer zawadi yake ya Sh Sh267,800,060.

Pamoja na kushinda kiasi hicho cha fedha, Laizer alikabidhiwa Sh267,800,060 kufuatia punguzo la kodi la Sh 53,559,612 kwa mujibu wa taratibu za serikali.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kuwa Laizer amefanikiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 13 za ligi mbalimbali sa soka duniani.

“Nampongeza Laizer kwa ushindi huu, amekuwa mmoja wa washindi wetu watano wa Jaackpot na wa pili kwa mwanamke kuibuka na ushindi wa kiasi kikubwa cha fedha, namshauri kuzitumia fedha hizo katika masuala la maendeleo,” alisema Tarimba.

Tarimba alisema kuwa SportPesa imedhamiria kubadilisha maisha ya watanzania kwa kujishindia fedha nyingi na ndiyo maana Jackpot yao imeanzia sh milioni 200.

“Tuna furaha kubwa kuwaongezea vipato Watanzania kupitia michezo yetu mbalimbali, unaweza kubashiri kwa mechi na kujipatia fedha,Lakini tumeenda mbali zaidi kwani tumekuwa tukitoa zawadi za fedha kwa wanaobashiri kwa usahihi mechi 10, 11 na 12 kupitia Jackpot Bonus na kuendelea kuwawezesha Watanzania,” alisema Tarimba.

Aliwaomba watanzania wenye vigezo vya kubashiri kufanya hivyo ilikujaribu bahati yao kwa kujishindia fedha.

Kwa upande wake, Laizer amesema kuwa atazitumia fedha hizo kuanzisha biashara ambazo zitamuongezea kipato.

Alisema kuwa yeye ni shabiki wa timu ya Arsenal na Simba na katika ubashiri wake, mume wake alimsaidia mechi moja tu kufikisha mechi 13 kwa mujibu wa taratibu.

“Mimi ni mfanyabiashara wa kuuza vitenge, sina mtaji mkubwa na biashara yangu ilikuwa kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida tu,” alisema Laizer.
Alifafanua kuwa atafanya utafiti wa kina kujua ni biashara gani ambayo ataifanya huku akifikiria kujenga nyumba na kusaidia familia yake.

“Sikuamini mara baada ya kuambiwa nimeshinda kiasi kikubwa cha fedha kupitia mchezo wa kubahatisha wa SportPesa”

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *