Ulaya yaibana Uturuki kisa sakata lake dhidi ya Syria

23 0

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaangazia kuimarisha vikwazo vya silaha dhidi ya mshirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO, Uturuki, katika upinzani wao dhidi ya mashambulizi yake dhidi ya vikosi vya Kikurdi katika taifa jirani la Syria.

Waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Stef Blok, amesema leo kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa kuingilia taifa jirani na Uturuki inapaswa kuzingatia sheria za kimataifa kama taifa lingine lolote.

Blok alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya mjini Luxembourg. Tayari Ujerumani, Ufaransa na Uholanzi zimesitisha hatua ya kuiuzia Uturuki silaha.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema kuwa anataka msimamo mkali dhidi ya mauzo ya silaha nchini Uturuki.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *