UN yaitaka Dunia kupinga vita baridi vya Marekani na China

13 0

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitolea wito dunia kusitisha vita baridi kati ya Marekani na China, na kusimamisha mizozo ili iweze kujikita katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19.

Guterres amesema dunia inachukua mwelekeo wa hatari sana, na kuonya kuwa haiwezi kuhimili mustakabali ambapo mataifa mawili yanayoongoza kiuchumi yanaigawanya dunia, kwa kila upande kuweka sheria zake za kifedha na za kibiashara.

Katibu mkuu huyo amesema kinachohitajika sio serikali ya dunia, bali mazingira mazuri ya uongozi. Guterres ameendesha kampeni ya kumaliza mizozo yote ya kivita duniani ili kupambana na janga la virusi vya corona, na ameitaja baadhi ya mifano ya mafanikio katika juhudi hizo, ikiwemo usitishwaji wa mapigano nchini Cameroon na Colombia.

Posted from

Related Post

DILI LA KASEKE YANGA LIMEIVA

Posted by - July 1, 2020 0
NA JESSCA NANGAWE UBORA wa winga wa Yanga, Deus Kaseke, umeendelea kumuweka kwenye viwango vya juu na sasa mabosi wa…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *