Usichokijua Kuhusu Kolabo ya Mondi na Alicia Keys

11 0Usichokijua Kuhusu Kolabo ya Mondi na Alicia Keys

IJUMAA iliyopita haikuwa siku ya hivihivi tu kwenye Bongo Fleva na muziki wa Afrika kwa ujumla. Ni siku ilipoandikwa historia mpya kwenye muziki huu baada ya kuachiwa kwa Album ya ALICIA ya mwanamuziki wa kiwango cha dunia kutoka nchini marekani, Alicia Augello Cook almaarufu Alicia Keys.

 

Hii ni albam yake ya saba katika kipindi chake chote cha kufanya muziki uliopendwa sehemu kubwa ya Sayari ya Dunia, yapata miaka 30 sasa akiwa kwenye gemu. Album yake ya kwanza ilikwenda kwa jina la Songs In A Minor, iliyoachiwa mwaka 2001. Album hii ilipotoka, ilifanya vizuri mno sokoni na kushika namba 1 kwenye US Billboard 200.

 

Pia album hii ilifanikiwa kibiashara kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 16 duniani kote na ikamfanya Alicia Keys kuwa Best-Selling New Artist na Best- Selling RnB Artist mwaka 2001. Album yake ya pili ilikwenda kwa jina la The Diary of Alicia Keys, iliyoachiwa mwaka 2003 na kuuza nakala

 

Album yake ya pili ilikwenda kwa jina la The Diary of Alicia Keys, iliyoachiwa mwaka 2003 na kuuza nakala milioni 8 duniani kote. Baada ya album hizi mbili, zilifuata nyingine za As I Am (2007), The Element of Freedom (2009), Girl on Fire (2012), Here (2016) na hii ya ALICIA ya mwaka huu (2020).

Albam ya ALICIA yenye ngoma kali 15, imekuwa gumzo mno Kibongobongo. Hii ni kwa sababu ndani yake kuna jina la mwanamuziki mkubwa kutoka Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika. Jina hili ni Diamond Platnumz, ambaye Alicia Keys amemshirikisha, kwenye ngoma inayokwenda kwa jina la Wasted Energy.

 

OVER ZE WEEKEND imefanya uchambuzi wa kolabo hii na hapa inakuletea usichokijua kuhusu muunganiko huo wa Diamond au Mondi na Alicia Keys;

Mondi ndilo jina pekee kutoka Afrika ndani ya album hii.

Uwepo wa Mondi ni ishara nzuri kwa muziki wa Bongo Fleva.

 

Sina hakika kama imetumika ladha halisi ya Bongo Fleva kwenye ngoma hiyo, lakini naamini lugha ya Kiswahili italibeba jina la Bongo Fleva. Kwenye album hii, Mondi amehusika kwenye ngoma hiyo namba 4 ya Wasted Energy.

 

Kizuri zaidi ni kwamba, ngoma hii ipo kwenye namba za juu kabisa. Ngoma hii inatabiriwa kufanya vizuri, kwani tayari imeanza kuweka rekodi kwenye mitandao ya kusikiliza, kutazama na kuuza na kununua muziki ya YouTube, Apple, Spotify, Mdundo, Boomplay, Audiomack, Vevo, Tidal, Deezer na mingine mingi.

 

Kikubwa usichokijua kuhusu Ngoma ya Wasted Energy ni kwamba, ndiyo ngoma ya pili kwa urefu; yaani ina dakika nyingi baada ya Ngoma ya Time Machine, yenye urefu wa muda wa dakika 4:30.

Wasted Energy yenyewe ina urefu wa muda wa dakika 4:19.

 

Wasted Energy ndiyo ngoma rasmi ya kwanza ya mwanamuziki wa Marekani kumshirisha msanii wa Bongo Fleva.

Pia Wasted Energy ni ngoma ya kwanza kuwa katika album ya mwanamuziki wa Marekani akiwa ameshirikishwa msanii wa Bongo Fleva.

 

Wabongo kama kawaida yao, wamekuwa wakiipamba albam hiyo kwa kuwa tu ndani yake yupo kipenzi chao, Mondi.

Mondi anazidi kuupa heshima muziki wa Bongo Fleva kutokana na kolabo hiyo na Alicia Keys. Ni hatua nzuri inayofungua milango katika soko la muziki wa Bongo Fleva kule Marekani.

 

Alicia Keys ambaye ni mke wa Producer Swizz Beatz, amewahi kutamba na ngoma kama; If I Ain’t Got You, Girl on Fire, Blended Family, No One, Fallin, In Common na nyingine nyingi, ambazo ni ngoma za levo ya dunia.

Katika kipindi alichofanya muziki, Alicia Keys ameshinda jumla ya tuzo 152 na nominations zaidi ya 200.

 

Ni miongoni mwa washindi wa Tuzo ya Grammy kwa mara 15 huku akiwa nominated mara 29. Ukiachana na hayo, Alicia Keys ana jumla ya wafuasi zaidi ya milioni 82.4 katika mitandao yake ya kijamii ya Instagram, Facebook na Twitter.

 

Wafuasi wote hawa 82.4M, wamecha-nganyika na mastaa wakubwa wa muziki duniani pamoja na sekta nyingine, wakiwemo; Ariana Grande, Nicki Minaj, Amandla Stenberg, Jessica Alba, Kehlani, Serena Williams, Serayah, Stephen Curry, Jordin Sparks, Dua Lipa, Chance The Rapper, 21 Savage, Camila Cabello, Cristiano Ronaldo, Tory Lanez, Marshmello, Shawn Mendes, The Rock, Post Malone, Aliya Janell, Meek Mill, Kevin Hart.

 

Ukweli ni kwamba, kwa wanaodhani Mondi amepata shavu la kitoto, wajitafakari mara mbilimbili. Alicia Keys ni mmoja wa wanamuziki wenye ushawishi mkubwa duniani.

 

Endapo ngoma hiyo itafanya poa, faida mojawapo kubwa ya Mondi kuwepo kwenye album hii, ni kwamba, huwenda tukaona msanii pekee kutoka Afrika Mashariki akiingia kwenye nomi-nation za tuzo kubwa kama Grammy na nyinginezo. Hongera Mondi; Mfalme wa Bongo Fleva!Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *