Uwoya: Niko Sawa na Tessy!

Malkia wa Bongo Movies, Irene Uwoya, ameweka wazi kuwa yuko sawa na aliyekuwa hasimu wake mkubwa, Tessy Abdul ‘Tessy Chocolate’.

 

Akizungumza na IJUMAA WIKIENDA juu ya ishu ya kupatana na Tessy, Uwoya amesema kuwa, yeye na Tessy hawajawahi kuacha kuongea na hawana ugomvi.

 

“Sijawahi kuacha kuongea na Tessy na hatuna ugomvi, tuko kwenye kundi moja la kampeni. Na sikuwahi kuchekelea matatizo aliyopitia (kuvamiwa kwenye saluni yake) kwa sababu ni mama kama mimi na sipendi kuona mtu kama yeye anapata tatizo halafu nikafurahia,” anasema Uwoya ambaye hivi karibuni alizindua kipindi chake kinachokwenda kwa jina la I AM EVERY WOMAN.

 

Uwoya na Tessy walikuwa ni mashosti, ambapo baadaye waliingia ndani ya bifu kubwa kwa kipindi kirefu, huku sababu ikisemekana ni kugombea mwanaume.

Stori: Happyness Masunga, BongoToa comment