Video: Walichosema Kocha wa Taifa Stars na SUDAN Mechi Ya Kesho

20 0

Video: Walichosema Kocha wa Taifa Stars na SUDAN Mechi Ya Kesho


KAIMU Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mrundi, Etienne Ndayiragije amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za wachezaji wa ndani Chan dhidi ya Sudan.
Stars kwa sasa inakibarua kigumu kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani kufuzu fainali za Chan zinazohusisha wachezaji wa ndani inayotarajia kufanyika nchini Cameroon mwaka 2020.

Kwa upande wake Kocha wa Sudan pamoja na nahodha wake wamesema wanafahamu itakua mechi ngumu kutokana na kikosi cha Tanzania kuwa kizuri lakini lengo lao kupata matokeo wakiwa ugenini.

Mechi itakuwa ya kwanza katika hatua hiyo kuwania kufuzu kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani CHAN.

Kumbuka Stars inakutana na Sudan kesho jumapili baada ya kazi kubwa ya kuwatoa Kenya.

Loading…

Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *