Video ya Offset akimsaliti mpenzi wake Cardi B yanaswa, Yeye ajibu tuhuma hizo – Video

27 0

Wikiendi hii rapper kutoka Marekani Kiari Kendrell Cephus alimaarufu Offset alikuwa nyumbani akitii agizo la #stayhome ikiwa ni kujikinga na maambukizi ya virusi hatari vya Corona.

Akiwa nyumbani na mpenzi wake Cardi B inaelezwa walikuwa wakicheza game na baada ya Cardi B kutoka Offset alionekana kuchat na mtu ambaye inaelezwa ni mchepuko huku akiendelea kucheza Video game na wakati huo huo akiwa LIVE kwenye Instagram,Offset alionekana pia akizungumza na simu lakini baada ya Cardi B kuingia chumbani aliificha simu hiyo na kuzua tetesi za kuwa rapper huyo alikuwa akizungumza na Mchepuko.

Baadaye aliiona video hiyo ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii baada ya watu kuidownload na kuisambaza huku wakitembeza kwa kutumia hashtag ya #OffsetMsaliti.

Baada ya video kusambaa na watu kushika neno moja tu la kuwa Offset ni msaliti, aliibuka IG na kujitetea. Alisema “Nafahamu nyote hampati chochote kwenye video ambayo nilikuwa naionesha nikicheza game na mpenzi wangu kuingia chumbani, Nikizungumzia hilo, mna fikra mbaya sana. Msizilete kwenye familia yangu. Kila kitu kipo sawa. Tuna miradi mikubwa sana tunafanya pamoja.” Alisema Offset

By Ally Juma.

 

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *