Vita Nzito! Aunty Amjibu Shamsa “Wewe Sio Msemaji wa Familia”

IKIWA ni saa chache baada ya mwanadada staa wa Bongo Fleva, Shamsa Ford kudai kuwa anashangazwa na rafiki yake Aunty Ezekiel kuwa na mahusiano na “watoto wa chekechea,” Aunty ameamua kuvunja ukimya na kumjibu.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aunty ameshusha ujumbe mzito kwa Shamsa, huku akimweleza kuwa yeye si msemaji wa familia yake.

 

“Anaekuheshimu mheshimu pia, sitaki kuongea sana, nakuheshimu Shamsa, naomba tuheshimiane, wewe sio msemaji wa familia yangu wala hayakuhusu ya familia yangu mbwa wewe, ya kwako mangapi au unavyofanyia kizani unaona watu hawakujui. SITAKI, SITAKI,” amesema Aunt.

 Toa comment