Vodacom Walivyozindua Duka Jipya Kariakoo

Mkuu wa Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Birgita Steven akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom imefanya jambo lao Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar, mkabala na Kituo cha Polisi kwa kuzindua duka lao jipya la bidhaa zao.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa duka hilo, Mkuu wa Vodacom Kanda ya Dar na Pwani, Birgita Steven amesema wameamua kufungua duka eneo hilo ili kuwapelekea huduma karibu wateja wa eneo hilo ambalo ni kitovu cha biashara hapa nchini.

Mkuu wa Vodacom Dar na Pwani, Birgita (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka hilo.

“Kama mnavyojua Vodacom ndiyo mtandao bora wa mawasiliano unaoongoza hapa nchini ambao mpaka umeshafikisha kwa wateja huduma ya 4G na 3G kwa asilimia mia moja.

“Hilo limesababisha wateja wa Vodacom kufurahia mawasiliano ya uhakika na spidi kali kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp, Instagram, Facebook, Twiter na mingineyo”. Alisema Birgita.

Wahudumu wa Vodacom wakimhudumia mteja aliyefika dukani hapo.

Birgita amesema kwa kutambua umuhimu wa kuendana na mambo ya kidijitali kwa watumiaji wa simu ndogo maarufu kama vitochi wamewawekea simu aina ya Smart kitochi ambazo zinauwezo kama simu janja zingine.

Birgita akimpa zawadi mmoja wa wateja anayetumia mtandao wa Vodacom kwa miaka ishirini sasa.

Pamoja na simu hizo, Birgita amesema kwenye duka hilo kuna bidhaa nyingine mbalimbali za Vodacom zenye ubora wa hali ya juu na kuwaomba wateja wafike kwenye duka hilo kujipatia huduma zao.
Toa comment