Vodacom Yaja Na Jimixie Bando

Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom leo imezindua huduma yake mpya iitwayo Jimixie Bando ambayo mteja wa kampuni hiyo ataweza kununua bado kwa kiasi chochote anachotaka kulingana na pesa yake.

Meneja Mkuu wa Kitengo cha Mikakati, Ufahamu na Utunzaji Wateja wa Vodacom, Jackson Walwa (kulia) alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Akizungumza na wanahabari kwenye duka la kampuni hiyo lililopo Mlimani City Dar, Mkuu wa Kitengo cha Mikakati, Ufahamu na Utunzaji Wateja wa Vodacom Tanzania, Jackson Walwa amesema kampuni hiyo imekuja na huduma hiyo kwa ajili ya kuboresha huduma za wateja wao.

Jackson amesema katika huduma hiyo mteja wao anaweza kujipatia bando la data, sms, muda wa maongezi au vyote kwa pamoja kwa muda anaotaka iwe bando la siku, wiki au mwezi.

Akielekeza jinsi ya kujiunga na bando hilo, Jackson amesema kwa mteja wa kampuni hiyo anachotakiwa ni kuingia *149*01# baada ya hapo unachagua Yakwako kisha unaingia Jimixie bando.

Naye Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa amesema huduma ni yakwanza hapa nchini ambayo itawapa unafuu wa matumizi wateja wao.

Mashuhuda wakiangalia tangazo jipya la huduma ya Jimixie bando.

Linda amesema dhamira ya kampuni hiyo ni kuleta mabadiliko chanya haswa ya kidigitali kwa wateja wao na kuwaasa waanze kujimixia ili wafurahie raha yake.

HABARI/PICHA: WAANDISHI WETU /GPL      Toa comment