Vurugu zinazoendelea katika mji wa Barcelona zapeleka kiungo wa Barcelona Ivan Rakitic kutembea kwa miguu – Video

18 0

Maelfu ya watu waliandamana jana katika mji wa Barcelona, kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama ya juu ya Uhispania dhidi ya maafisa tisa wa jimbo la Catalonia walioongoza vuguvugu la kutaka uhuru wa jimbo hilo lenye mamlaka ya ndani.

Maafisa hao walihukumiwa vifungo vya kuanzia miaka 13 jela kwenda chini, adhabu ndogo ikilinganishwa na miaka 25 iliyokuwa imependekezwa na upande wa waendesha mashtaka kwa aliyekuwa makamu Rais wa Catalonia, Oriel Junqueras.

Mahakama hiyo ilimhukumu Junqueras kifungo cha miaka 13, baada ya kumkuta na hatia ya uhaini na matumizi mabaya ya raslimali za umma.

Waliokuwa mawaziri katika serikali ya jimbo hilo wamepewa adhabu ya kifungo cha miaka 12 jela. Kutangazwa kwa hukumu hiyo kulifuatiwa na maandamano makubwa katika mji mkuu wa Catalonia, Barcelona, ambapo kwa muda mfupi waandamanaji walivifunga vituo vya treni na uwanja wa ndege.

Katika vurugu hizo nyota wa Barcelona Ivan Rakitic amelazimika kuondoka uwanja wa ndege wa Barcelona kwa miguu kufuatia maandamano yanayoendelea katika jimbo la Catalonia.

Maelfu ya waandamanaji wanaendelea kumiminika katika mitaa ya Barcelona, kupinga hukumu iliyotolewa Jumatatu na mahakama kuu ya Hispania dhidi ya viongozi wa Kikatalani walioshinikiza jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania.

Inaripotiwa kwamba waandamanaji hao wana mpango wa kutumia mechi ya El Clasico itakayochezwa pale Camp Nou tarehe 26 mwezi huu kama sehemu ya kupinga hukumu hiyo, kwani itakuwa mechi inayofuataliwa ulimwenguni kote.

By Ally Juma.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *