Vyuo na shule bado vyabaki kufungwa hadi mwakani Kenya!

6 0

Katika hotuba ya raisi kuhusu kukabidhi janga la Corona nchini Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye ndie raisi wa taifa hili jirani jana alitoa maagizo kwamba vyuo vikuu, shule za upili na msingi vitabaki kufungwa hadi mwakani ili kuipatia serekali nafasi ya kutathimni jinsi ya wanafunzi na walimu watakavyo ishi na kujilinda kuotokana na maambukizi ya COVID19.

Hatimae maeneo ya burudani yamefunguliwa huku marufuku ya kutotumia pombe kwenye baa ikifutiliwa mbali. Na pia amri yakutotoka nje usiku, masaa yake yameongezwa hadi saa tano ndio mwisho kwa siku 30 sijazo, ikiwa awali ilikua mwisho ni saa tatu usiku. Wakenya wameonekana kufurahishwa na jambo hili huku wengi wakiomba amri yakutotoka nje usiku ifutiliwe mbali kabisa. Hata hivyo Uhuru Kenyatta amewaonya wanasiasa kuwa mstari wambele katika kupambana na corona kwa kuepuka kujifanyia mikutano isio na misingi kwa kujitakia kujiongezea umaarufu.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *