Wadau wa burudani na wasanii waliogombea Ubunge 2020, Mwana FA, Babu Tale na Shigongo kidedea, Wakazi, Sugu, Profesor Jay chali

10 0

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, amemtangaza Mwana Fa wa CCM kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 47,578 na kumshinda Yosepher Komba wa CHADEMA aliyepata kura 12,034.

Mwana Fa anaungana na wasanii wengine ambao waliingia Bungeni kama Joseph Mbilinyi aliyeshindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini na Joseph Haule ‘Prof Jay’ aliyeshindwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Mikumi.

Watu wengi wamempongeza Mwana Fa kwa matokeo hayo akiwemo mtu wake wa karibu na msanii AY ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa “Ni Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma ‘Mwana Fa’ kwenye moja na mbili hongera,  hatimae ndoto yako ya muda mrefu ya kuwatumikia ndugu zako wa Muheza, kila la kheri mwanangu maana nakuaminia kwenye mipango ya kimaendeleo, Mungu ni mwema sana sasa kazi ianze

Lakini pia Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buchosa amemtangaza Mgombea Ubunge Jimbo hilo Kupitia CCM Erick Shigongo @ericshigongo kuwa mshindi kwa kupata kura 79,950 akifuatiwa na Abbas Mayala (CHADEMA) kura 11,285.

Watu wengine waliopo kwenye tasnia ya Muziki ni pamoja na Babu Tale aliyeshinda katika jimbo la Morogoro Kaskazini huku Profesor Jay jimbo la Mikumi, Joseph Mbilinyi Sugu  jimbo la Mbeya mjini na wote walikuwa Chadema na wameshindwa kwenye Ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu 2020.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *