Wagonjwa wa Corona Kenya Wafika 50

WAZIRI wa Afya wa Serikali ya Kenya, Mutahi Kagwe jana Jumatatu, Machi 30, alitangaza wagonjwa nane zaidi wa ugonjwa wa virusi vya corona COVID-19 na kufanya idadi ya wagonjwa nchini humo kufikia 50.

 

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Waziri Kagwe alisema kuwa wagonjwa hao nane wameambukizwa virusi vya corona ndani ya nchi na kutoa tahadhari ya ugonjwa huo kuenea ndani kwa kuwa hakuna maambukizi mapya kutoka nje.

 

Mpaka Jumamosi, Kenya ilikuwa na wagonjwa 38. Juzi Jumapili Waziri Kagwe alitangaza wagonjwa wapya wanne na kufanya idadi kufikia 42, hivyo idadi ya wagonjwa wapya 12 nchini humo imetangazwa ndani ya siku mbili tu. Mtu mmoja tayari amepoteza maisha nchini humo kutokana na virusi hivyo.

 
Toa comment