Wahitimu St Mark’s Waaswa Kutojiingiza Kwenye Utumiaji Dawa za Kulevya

Wazazi na walezi wametakiwa kutokimbilia shule zenye ufaulu  kwa ajili ya kuwapeleka watoto  wao na kuaswa kuwatafutia shule zitakazowajenga kimaadili ili wasijekujiingiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya.

Akizungumza wakati wa mahafali ya 17 Mkurugenzi Mtendaji wa shule  ya St. Mark’s Peter alisema kuwa baadhi ya wazazi, wanakimbilia shule zenye ufaulu lakini wanashindwa kuelewa kuwa kuna shule zinaufaulu lakini haziwajengei watoto maadili.

” Kabla ya kumpeleka mtoto shule mzazi ufuatilie shule hiyo ina maadili au haina na Kama haina usikimbilie sifa za ufaulu  pekee na ukampeleka mtoto,” amesema.

Aliongeza kuwa kama mtoto atakuwa hana maadili na akafaulu vizuri mitihani yake lakini anapopata ajira hawezi kufanya kazi vizuri kutokana na kutokuwa na maadili mema.

Aliendelea kwa kusema shule yao imeanzisha sera ya usalama kwa watoto wakiwa ndani ya shule na nje ya shule.

” Tumeanzisha sera yetu tunawalinda  watoto  na matendo ya usalama nje na ndani ya shule.

“Mtoto akitoa taarifa kuwa nyumbani  ananyanyaswa tunafuatilia taarifa hizo  ili tuweze kuzishughulikia.

“Naipongeza Serikali   ya awamu ya tano  kwa kuboresha elimu  ambapo kwa sasa  watoto wengi wanapata elimu na natoa nasaha kwa wahitimu maadili mliyoyapata hapa mkayandeleze mnapokuwa  mitaani,”alisema mkurugenzi huyo.

Aidha amewataka wahitimu hao wasijiingize  katika makundi yasiyofaa ikiwemo na kujihusisha na matumizi ya madawa kulevya.
Toa comment