Wajue Matajiri Wakubwa Zaidi Duniani

MNAMO mwaka jana, utajiri unaomilikiwa na  mabilionea 10 wakubwa zaidi duniani umepanda na kufikia zaidi ya Dola bilioni 76.

Pamoja na matatizo mbalimbali katika masoko ya biashara, matajiri wengi wakubwa zaidi duniani wameshuhudia utajiri wao ukipanda licha ya kuwepo kwa janga la ugonjwa wa Covid-19.

Chini ni orodha ya mabilionea 10 wakubwa zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes,  likionyesha utajiri wao kutoka Machi 5, 2019 hadi Aprili 22, 2020. Hii ni pamoja na mabadiliko ambapo baadhi yao utajiri umeshuka.

Na. Jina Utajiri 2020* Utajiri 2019* Badiliko 2019-2020
#1 Jeff Bezos $145B $131B +$14.1B
#2 Bill Gates $104B $97B +$7.1B
#3 Bernard Arnault & Family $92B $76B +$15.5B
#4 Warren Buffett $73B $83B -$9.1B
#5 Mark Zuckerberg $69B $62B +$6.5B
#6 Larry Ellison $66B $63B +$3.4B
#7 Steve Ballmer $63B $41B +$21.3B
#8 Amancio Ortega $61B $63B -$2.2B
#9 Larry Page $58B $51B +$7.6B
#10 Jim Walton $57B $45B +$12.0B
Ongezeko la Jumla +$76.2B

Chanzo: Forbes – *Hadi April 22, 2020 , Kuanzia March 5, 2019

Mkuu (CEO)  wa kampuni la Microsoft, Steve Ballmer, utajiri wake umeongezeka kwa zaidi ya Dola bilioni 21 tangu Machi 2019 ambapo Warren Buffett, utajiri wake umepungua kwa zaidi ya Dola bilioni 9, wakati Mark Zuckerberg utajiri wake ukizidi kuimarika.

Matajiri kuongezeka kwenye listi

Wakati biashara ikindelea duniani, kuna matajiri ambao wanategemewa kujiunga na orodha ya mabilionea wakubwa zaidi duniani nao ni:

Na. Jina Utajiri Chanzo cha Utajiri
#1 Eric Yuan $7.8B Zoom
#2 Anthony von Mandl $3.9B Mark Anthony Brands
#3 Larry Xiangdong Chen $3.6B GSX Techedu
#4 Dmitry Bukhman $3.1B Playrix
#5 Igor Bukhman $3.1B Playrix
#6 Sun Huaiqing $3.0B Guangdong Marubi Biotechnology
#7 Forrest Li $2.4B Sea Group
#8 Byju Raveendran $1.7B Byju’s
#9 Jitse Groen $1.5B Takeaway.com
#10 Qian Ying $1.5B Muyuan Foods

*Kwa mujibu wa kuanzia Aprili 22, 2020Toa comment