Waliomuua Dkt. Mvungi Wahukumiwa Kifo

WATU watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya aliyekuwa mwanasheria maarufu nchini na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Sengondo Mvungi.

Hukumu hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam ambapo pia mahakama imemwachia huru mshitakiwa mmoja.

Mvungi alivamiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Novemba 3, 2013, na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, jambo lililosababisha kifo chake akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.Toa comment