Walionaswa Wakijiunganishia Umeme Wapandishwa Kortini – Video

WATU wawili na wafanyabiashara wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Nassoro Halfa (40)na Mussa Saidi (49) wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Kusomewa Shtaka moja la Uhujumu uchumi.

 

Akiwasomea hati ya mashtaka wakili wa Serikali Mwandamizi, Maternus Marando Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Matembele Kassian amesema kuwa washtakiwa wote kwa makusudi na kwa nia ovu maeneo ya mikocheni Dar es Salaam waliingilia miundombinu ya Mali ya Shirika la Umeme Tanesco inayotoa huduma kwa kujiunganishia umeme kinyume cha sheria.

 

Baada ya Kusomewa Shtaka lao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi mpaka kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Baada ya Kusomewa Shtaka linalowakabili Hakimu Matembele amesema kuwa dhamana kwa washtakiwa ipo wazi na wametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja ameitakiwa kusaini Bondi ya Mil 5, kuwa na barua kutoka kwa waajiri wao, kuwasilisha hati zao za kusafiria au kitambulisho cha Taifa kila mmoja na Sharti lingine ni kutokusafiri nje ya mkoa wa Dar bila kupata kibali kutoka mahakamani.

 

Hata hivyo washtakiwa wameshindwa kutimiza mashti na wamepelekwa rumande hadi hapo watakapokidhi vigezo hivyo na kesi imeahirishwa hadi Septemba 10 mwaka huu upelelezi upo katika hatua nzuri kukamilika.Toa comment