Wamepotea, Wanawatafuta Wazazi Wao

 

Usiku wa kuamkia leo Agosti 29, 2020 majira ya saa 08:00, Hospitali ya Taifa Muhimbili (UPANGA) imewapokea binti Aurelia Mkula (16) akiwa na mtoto wa kiume anayeitwa Ivan (1) ambao wameletwa na Polisi wa Kituo cha Mwongozo (Ubungo-External).

 

Bi. Aurelia anasema yeye ni dada wa kazi hivyo jana saa 05:00 asubuhi alitumwa na mama wa mtoto Bi. Belinda Swai kwenda kwa rafiki yake ambaye yuko jirani na wanakoishi maeneo ya Ubungo.

 

Wakati anarudi nyumbani ALIPOTEA NJIA NA KUSHINDWA kutambua alikotokea. Amesema alijaribu kuuliza watu njiani mahali alipotokea bila mafanikio ndipo msamaria mwema alipojitokeza na kumpa nauli ya BODABODA ili ampeleke kituo cha Polisi.

 

Hivyo, tunao hapa Hospitalini tunatafuta wazazi wa watoto hawa. Aurelia amesema mtoto Ivan ana wazazi wake wote wawili baba yake yuko Bukoba kikazi na mama yake yupo hapa Dar Es Salaam. Naomba wazazi wa watoto hawa wajitokoze ili wawachukue.

 

Wasiliana nami;
Aminiel B. Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Hospitali ya Taifa Muhimbili
0784 648636

DAR ES SALAAM 29.08.2020Toa comment