Wana Vipaji Vikubwa, Tatizo Nyota!

2 0Wana Vipaji Vikubwa, Tatizo Nyota!

 

KWENYE gemu la muziki, mbali na kufanya kazi nzuri za kuwafi kia mashabiki, ila pia inabidi msanii akubalike kwa mashabiki zake.

 

Wapo wasanii ambao wamekuwa wakikubalika kwa mashabiki zao na nyota zao kung’aa kila pande, ila wengine wamekuwa wakifanya kazi nzuri, bali nyota zao zimekuwa zikiwaangusha na kuwafanya wasifi ke mbali zaidi.

Makala haya yanakuletea wasanii ambao wana vipaji vikali, ila tatizo limekuwa kwenye nyota.

 

BEN PAUL

Bernad Paul ndilo jina halisi. Ben ni mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva na RnB. Nyimbo nyingi anazoimba na uimbaji wake, ni mzuri, lakini imekuwa ni vigumu kutoboa kimataifa, pia hata kwa tuzo za hapa Bongo.

Ben Pol ametamba na ngoma kali kama Jikubali, Unanichora, Sophia, Pete, Moyo Mashine na nyingine nyingi.

 

BARNABA
Barnaba Elias ni zao kali kutokea Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), pia ni mwanamuziki mzuri, unaweza kusema anamshinda hata Diamond kiuwezo, kwani amefanya kazi kadhaa zikakubalika.

Mbali na uimbaji wake, ni mtunzi mzuri wa nyimbo mbalimbali na wasanii wenzake. Barnaba amejaaliwa kipaji kingine cha kutumia vyombo vya muziki, tofauti na wanamuziki wengi ambao wanajua kuimba tu.

 

Barnaba amefanya vizuri kwa nyimbo zake kama Suna, Siri aliofanya na Vannesa Mdee, Wahalade ambayo ilipendwa sana na mashabiki wengi, Sichomoi, Washa, Mapenzi Jeneza, Chausiku, na nyingine nyingi.

 

BELLE 9

Wimbo wa Sumu ya Penzi ndiyo uliomtambulisha kwenye anga la muziki. Abednego Damian ‘Belle 9’ ndiyo jina lake halisi, jamaa ana kipaji na uwezo mkubwa wa kuimba.

 

Ngoma zake zingine zilizotikisa ni pamoja na Shauri Zao, Listen, Wewe ni Wangu, Maole na nyingine, ambapo kwa sasa anatamba na ngoma ya Umefanana Naye, lakini ameshindwa kutoboa kimataifa kama walivyo akina Ali Kiba na Diamond wakati ni mwanamuziki mzuri.

 

RICH MAVOKO

Richard Martin almaarufu Rich Mavoko au Messi wa Bongo Fleva, ametambulika na kufanya poa na ngoma kama Pacha Wangu, Marry Me, Rudi, Roho Yangu, Moyo na nyingine kali.

 

Rich ni msanii mwenye kipaji kikali na aliwahi kusajiliwa na lebo kubwa ya muziki sasa alivyokuja kusimama tena na kuachia Mini Tape yake yenye ngoma nane.

 

MO MUSIC

Moshi Katemi ni jina lake halisi, ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye amefanya ngoma kali kama Basi Nenda, Simama na Nitazoea, Boda Boda na nyingine kali.Mo ni msanii mwenye ngoma kali na sauti tamu na ya kipekee, lakini ameshindwa kutoboa hapa nyumbani na hata anga za kimataifa zaidi, labda sababu ni masomo, kwani anafanya muziki na masomo kwa wakati mmoja.

 

BARAKA THE PRINCE
Baraka Andrew ni msanii mwenye kipaji kikali ambacho kama angetulia vizuri, ilikuwa ni
rahisi kutoboa kimataifa zaidi. Baraka amefanya poa na ngoma kali kama Siachani Nawe, Jichunge, Nisamehe, Acha Niende, Siwezi na nyingine kali.

Baraka aliwahi kuwa chini ya lebo kubwa ya muziki ya Rock Star akiwa pamoja na Ali Kiba na Ommy Dimpoz, lakini ameshindwa kutoboa kutokana na nyota yake kufi fi a mpaka sasa.

Alikaa kimya kwenye gemu, lakini baadaye akaamka japo si kwa yale manjonjo na kusikika zaidi kama ilivyo kwa wasanii wengine.

 

STEVE RNB

Steve RnB, ni msanii mwenye sauti kali na kipaji cha hali ya juu. Amefanya ngoma kali kama Jambo Jambo, Huyu Demu, Why, One Love na nyingine kali. Ngoma zake zina ubora, lakini ameshindwa kutoboa kimataifa na hata hapa nyumbani.

 

KASSIM MGANGA

Tajiri wa mapenzi Kassim Mganga, ni msanii mkali kutoka kwenye kundi la muziki la Tip Top Connection. Kassim amefanya poa na ngoma kali kama Amore, Awena, I love You, Haiwezekani, Solemba, Somo, Subira na nyingine kali ambazo zimekuwa zikifanya poa, lakini tatizo nyota.

 

RAMA DEE

Msanii mwingine anayesifi ka kuwa na kipaji kikali na ameweza kuuenzi muziki wa RnB halisi tangu aanze. Rama alitambulika na ngoma kali ya Kuwa na Subira na ilifanya poa na kumtambulisha poa.

 

Baadaye akatikisa tena na ngoma nyingine kama Kipenda Roho, Usihofie Wachaga, Kwa akili yangu, Protocol na nyingine kali. Nyota ya Rama imeshindwa kung’aa, kiasi kwamba mpaka sasa amekuwa kimya kwenye utoaji wa kazi zake.

 

USHAURI

Kwa wasanii, ni bora kujituma na kuzidi kutafuta mianya ya kimataifa, maana kazi nzuri na yenye ubora, hutambulika kimataifa.

MAKALA: HAPPYNESS MASUNGA, RISASIToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *