Wananchi Wataka Kufahamu Atakayowafanyia Shigongo Buchosa

1 0Wananchi Wataka Kufahamu Atakayowafanyia Shigongo Buchosa

 

WAKATI mchakamchaka wa kampeni ukiendelea kupamba moto katika maeneo mbalimbali huku wagombea urais, ubunge na udiwani wakinadi sera zao ili wachaguliwe na wananchi kuwaongoza katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020,  Jimbo la Buchosa nako mambo yamenoga.

 

Wananchi wa vijiji mbalimbali vya jimbo hilo wamejitokeza kuchukua jarida maalum lenye mambo mazito ndani yake ambayo mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James,  anayaahidi kuyafanya endapo watampa ridhaa hiyo ya kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

 

Wakizungumza na www.globalpublishers.co.tz, baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa jarida hilo ni muhimu kwao kwani ni rahisi kusoma na kuelewa ahadi za mgombea wao, Shigongo,  na namna ambavyo atazitekeleza na kuwaletea maendeleo.

 

“Ujue huku kwetu ni kijijini, hivyo jarida hili linaturahisishia kusoma, kuelewa na kuchambua sera bora za kiongozi tunayemtaka.

 

“Pia ni rahisi mimi kulisoma na kuipelekea familia yangu ama rafiki zangu nao wakasoma hata kama hawakuwepo kwenye mkutano wa kampeni basi watakuwa wameelewa kila kitu ambacho Shigongo amedhamiria kutufanyia wananchi wa Buchosa,” alisema Mpogomi John Bujingi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mwangika.

 

“Sisi akina mama wa Buchosa tunazo changamoto nyingi  zinazotukabili, kwenye  kilimo, vikundi, biashara,  na mengine  mengi.  Katika  jarida hili  tumeona  kuna  mambo  mengi  ambayo  Shigongo  ameyaainisha  kama  vipaumbele  vyake  iwapo  atachaguliwa.  Kwa  kweli yanatugusa sana sisi  akina  mama;  ninawashauri  wananwake  wenzangu  na Wana-Buchosa  wenzangu  wasome jarida hili,  ambapo wataelewa  nini  ambacho  mtu  huyu  amedhamiria  kutufanyia,” alisema  Mama Ng’weshemi.

 

Jarida hilo tayari limeshagawiwa katika baadhi ya wananchi wa vijiji vya Bulyahilu, Iligamba, Lushamba, Kanyala na Itulabusiga.

Pia ndani ya jarida hilo huzungumziwa maisha halisi ya Shigongo na namna ambavyo atahakikisha anatatua changamoto za wananchi wa jimbo hilo kupitia ushirikiano wao endapo watampa ridhaa ya kuwa msemaji wao ndani ya Bunge la Tanzania.

Kampeni za Shigongo zilizokuwa zizinduliwe Alhamisi ijayo, Septemba 24, 2020, zimesogezwa mbele mpaka Ijumaa, Septemba 25, 2020, ambapo zitafanyika katika Viwanja vya Nyakaliro kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 12:00 jioni na mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa.

 

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERSToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *