Wanne Kortini kwa Tuhuma za Kuendesha Bisahara ya Madawa

11 0Wanne Kortini kwa Tuhuma za Kuendesha Bisahara ya Madawa

WATU wanne wamepandisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwemo kosa la kuendesha biashara haramu ya dawa za kulevya aina ya heroine kiasi cha kilogramu 51.47 na utakatishaji fedha.

 

Washitakiwa hao ambao ni ERNEST MICHAEL, SALUM JONGO, AMIN SEKIBO na TATU NASSOR wakazi wa Mbezi Jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika mahakama hiyo hii leo Septemba 16, 2020 na kusemewa mashtaka yao na wakili wa Serikali Mkuu, PAUL KADUSHHI akisaidiwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali WANKYO SIMON mbele ya Hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo CASSIAN MATEMBELE.

 

Awali akiwasomea hati ya mashitaka Wakili wa Serikali Mkuu, PAUL KADUSHI amedai kuwa washitakiwa hao katika tarehe tofauti kati ya Septemba 8, 2020 maeneo ya Vetenari Jijini Dar, washitakiwa walikamatwa na Kilogram 51.47 za dawa za kulevya aina ya heroin.

 

Katika shitaka la pili Wakili KADUSHI amedai kuwa Septemba 1 na 8, 2020 Washitakiwa hao wanadaiwa kujihusisha na utakatisha wa fedha zilizotokana na biashara haramu ya dawa za kulevya wa zaidi ya shilingi milioni sitini na mbili.

 

Katika shitaka la pili washitakiwa wote kwa pamoja kati ya Septemba 1 na 8 mwaka 2020 katika Jiji la wa Dar es Salaam walitenda kosa la utakatishaji fedha haramu kwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu fedha za kitanzania shilingi milioni 62,370,000, fedha za Msumbiji 7,370, Fedha ya Kenya shilingi 400, na magari manane ya aina tofauti.

 

Katika shitaka la tatu ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam kati ya Septemba 1 na 8 mwaka 2020 inadaiwa washitakiwa walitenda kosa la kuongoza genge la uhalifu kwa kusafirisha dawa za kulevya aia ya heroine kilo 51.47.

 

KADUSHI amedai kuwa Washitakiwa hao pia Septemba Mosi mwaka huu Jijini Dar es Salaam katika maeneo tofauti walikutwa wakimiliki Magari nane ya kifahari, nyumba tatu, laptop moja aina ya Apple na shamba la hekari kumi na tisa ambavyo wanadaiwa kujipatia kupitia biashara haramu ya dawa za kulevya.

 

Aidha, Wakili PAUL KADUSHI amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo kwenye hatua za Mwisho kukamilika hivyo kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septamba 30 mwaka huu na washitakiwa wote wamerudishwa gerezani.

Salim Abdurahmani  – Global TV Online

 Toa comment

Posted from

Related Post

Kane apelekwa Man United kilazima

Posted by - July 29, 2020 0
MANCHESTER, England KAMA Manchester United wanahitaji kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao, basi wameshauriwa kuifukuzia saini ya straika…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *