Watanzania msisafiri bila vibali – RC Mtwara – Dar24

3 0

Watanzania wametakiwa kutosafiri kuelekea nchi jirani ya Msumbiji, bila kuwa na vibali au nyaraka halali zitazowatambulisha utaifa wao, na kutumia vivuko rasmi vinavyotambulika ili kuepuka madhara ya kiusalama yanayoweza kujitokeza.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa, amekanusha taarifa zinazodai kuwepo kwa raia wa Msumbiji wanaokimbilia katika maeneo ya jirani na mpaka wa Tanzania na wengine kushambuliwa.

Byakanwa amesema kuwa suala la kuwataka kutumia utaratibu huo linalenga kuimarisha ulinzi wa mipaka na kuendelea kujiridhisha juu ya kumbukumbu sahihi ya watanzania waliotoka na kuingia nchini.

Amesema kuwa kutokana na kukauka kwa maji katika mto Ruvuma, mpaka wa Tanzania na msumbiji unapitika kwa urahisi hata kwa kutembea na miguu.

Hata hivyo Byakanwa amekanusha uwepo wa taarifa kuwa machafuko yanayoendelea Msumbiji yameiathiri Tanzania, na kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini vimejipanga imara kulinda usalama wa mipaka yake.

Rweyemamu: Hatutaidharau Mtibwa Sugar

Comments

comments

Posted from

Related Post

Winga Mzambia Mambo safi Yanga

Posted by - January 14, 2020 0
Winga Mzambia Mambo safi Yanga January 14, 2020 by Global Publishers ACHANA na uwezo mkubwa aliouonyesha starika Muivory Coast, Yikpe…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *