Watanzania Waliokutwa na #Covid19 Wazuiwa Kuingia Kenya

Serikali ya Kenya imewarudisha Watanzania wawili jana Mei 12, waliokuwa wanataka kuingia Kenya baada ya Watanzania hao kuthibitika kuwa na #COVID19 katika mpaka wa Isebania.


Katibu Mkuu (Utawala) wa Wizara ya Afya, Dkt. Rashid Aman amesema; “Tunawapima Watanzania wanaotaka kuvuka mpaka, lakini tunawapima wakiwa kwao na kisha tunawashirikisha majibu.”


Aidha, #Kenya imepinga taarifa zilizokuwa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa imefunga mipaka yake ya kutoka #Tanzania ya Namanga (Arusha) na Horohoro (Tanga).

Msemaji wa Serikali ya nchi hiyo, Cyrus Oguna amesema hawawezi kufunga mipaka bila kufuata utaratibu, kama ikifikia hatua hiyo itatangazwa kwa Umma kupitia Mamlaka za Serikali.Toa comment