Watumiaji Mabando Ya Tigo Sasa Waula

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo leo imezindua huduma yake mpya iitwayo Chukua Kilicho Chako ambayo itamuwezesha mtumiaji wa bando la kampuni hiyo kuokoa bando lake kwa kujiongezea bado jipya.

Mambo yakiendelea mapaparazi nao kazini.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kwenye ofisi za kampuni hizo zilizopo Makumbusho Jijini Dar, leo Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Woinde Shisael alisema;

“Hii ni huduma yetu mpya kabisa hapa nchini ambayo itamuwezesha mtumiaji wa bando letu kuokoa bando lake lisiishe muda wake kwa kuongeza bando lingine kama hilo.

“Unachotakiwa kufanya kama ulikuwa na bando la wiki likiwa linakaribia kuisha muda wake unapoongeza bando lingine kama hilo basi kiasi kilichobakia kinaungana muda wa kumalizika wa bando jipya ulilojiwekea na hivyo kuokoa muda wake wa kutumika”. Alimaliza kusema Sishael.

Meneja wa Huduma za Internet wa Tigo, Nevonaeli Eliakimu akifafanua jambo.

Naye Meneja wa Huduma za Internet wa kampuni hiyo, Nevonaeli Eliakimu amesema kampuni hiyo imeamua kufanya hivyo baada ya kupitia changamoto za wateja wao na kuamua kuziboresha kwa mtindo huo ambapo wengi mabando yao yalikuwa yakiisha muda wake bila kuyamaliza.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPLToa comment